Kukuta Dereva wa pikipiki amevaa helment au kofia ngumu hiyo ni kawaida hata kwa mwendesha baiskeli pia ni kawaida sababu ya kuzuia kuumia kichwa wakianguka kutokana na aina ya vyombo vya usafiri wanavyotumia, lakini kwa Dereva wa gari kuvaa helment ni jambo ambalo ushangaza na kutoa maswali mengi.
AyoTV na millardayo.com inakukutanisha na Dereva wa basi la Fatima Express linalofanya safari zake kutoka Mkoa wa Njombe kwenda Songea Mkoani Ruvuma anayefahamika kwa jina la Erick yeye huvaa helment wakati anaendesha gari hatujui sababu kubwa kwanini anavaa lakini amekubali kukaa nasi kutuelezea kwanini anavaa helment ya pikipiki wakati anaendesha gari.
RC MWANRI AMUWASHIA MOTO MHINDI WA MRADI WA BIL. 602 “NAPATA SHIDA MOYONI“