Shirikisho la soka Tanzania TFF leo Ijumaa January 18 2019 likiwa bado linadaiwa kuwa katika changamoto ya kumtafuta mdhamini mkuu wa Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2018/2019, limewatangaza Biko Sports ambayo ni kampuni ya michezo ya ubashiri kuwa mdhamini tuzo za mchezaji bora wa mwezi na kocha bora.
Biko Sports katika kipindi chote cha msimu wa 2018/2019 kilichobakia watatoa fedha kwa mchezaji bora wa mwezi na kocha bora ambapo kila mmoja ambapo atapatiwa Tsh milioni 1, mbali na fedha hizo pia wadhamini hao watatoa tuzo maalum za mchezaji bora na kocha bora wa kila mwezi.
TFF ina utaratibu wa kuwazawadia wachezaji bora na makocha wa kila mwezi pamoja na wale wa msimu mzima wa Ligi Kuu, TFF inayoendelea kutafuta mdhamini wa Ligi Kuu imeendelea kuongeza wadhamini wadogo wadogo (Co-Sponsors) wakiwa bado hawajapata mdhamini Mkuu, hata hivyo Biko na waungana na KCB ambao tayari walishadhamini Ligi miezi kadhaa nyuma.
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”