Mechi namba 153- Desemba 7, 2018: Singida Utd 0 vs Stand Utd 1. Kocha Msaidizi wa Singida Utd, Shadrack Nsajigwa amefungiwa mechi mbili na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kuondolewa kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kupinga maamuzi ya Mwamuzi.
Mechi namba 165- Desemba 15, 2018: Ndanda 1 vs African Lyon. Kocha wa makipa wa African Lyon, Juma Bomba amefungiwa mechi mbili na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kuondolewa kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kupinga maamuzi ya Mwamuzi.
Mechi namba 180- Desemba 30, 2018: Simba 3 vs Singida Utd 0. Klabu ya Singida Utd imetozwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kutokana na timu yake kutoingia kwenye chumba cha kubadilishia (changing room), na badala yake kuingia kwenye chumba cha waandishi wa habari, jambo lililosababisha usumbufu kwa waandishi wa habari.
Mechi namba 192-Januari 5, 2019: Mbao 0 vs Alliance FC 0. Klabu za Mbao na Alliance FC zimepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kila moja kwa kushindwa kuingiza timu za U20 kwenye mechi ya utangulizi, pia Alliance FC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia, hivyo kufanya timu yao ikaguliwe nje ya vyumba.
Mechi namba 195- Januari 6, 2019: Biashara Utd 0 vs Singida Utd 0. Mchezaji wa Singida Utd, Godfrey Mwashiuya amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga mpinzani wake ngumi kwa makusudi wakati mpira ukiwa umesimama.
Mchezaji wa Singida Utd, Rajab Zahir amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kuoneshwa kadi nyekundu mara baada ya mchezo kumalizika kwa kosa la kutoa lugha ya matusi kwa Mwamuzi na kutaka kumpiga.
Mechi namba 124- Novemba 3, 2018: JKT Tanzania 0 vs Simba 2. Mwamuzi Msaidizi namba mbili Mashaka Mwandembwa amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kutafsiri vizuri sheria ya kuotea. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39 ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi. Pia Mwamuzi Mbaraka Rashid amepewa Onyo kwa kutokuwa makini wakati wa akichezesha mechi hiyo.
IMETOLEWA NA TFF
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”