Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Sheria TAKUKURU, Donasian Kessy amesema wamewasilisha nyaraka za vigogo hao ili kesi zao zianze kusikilizwa mahakamani hapo baada ya kukamilika upelelezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kessy amezitaja kesi hizo kuwa ni ile inayomkabili aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘ TRA’, Harry Kitilya na wenzake pamoja na ile inayomkabili Mohammed Yusufali ambaye alitajwa na Rais John Magufuli kuwa anaiibia serikali Mil.7 kwa dakika.