Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amelitumia jukwaa la kilele cha Siku ya Sheria kuitaka Mahakama na Vyombo vinavyotoa huduma kwa wananchi kutenda haki na kutojihusisha na rushwa.
“Rushwa inapofusha ukishapokea unakuwa kipofu ukiulizwa swali unasema kuhusu nini, ukikaa katika nafasi za kufanya maamizi makubwa lazima ujitambue kuwa mtu mtakatifu” RC Mwanri