Ipokee hii kutokea Mkoani Tabora ambapo Profesa Juma Kapuya aliyekuwa Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa amefunga ndoa Jumapili ya February 17,2019 na mpenzi wake Mwajuma Mwiniko mwenye umri wa miaka 25 huko Urambo.
Prof. Juma Kapuya kama utakuwa unakumbuka alikuwa waziri wa ulinzi na mbunge wa Urambo Tabora wakati wa utawala wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Prof Kapuya kwa sasa amestaafu na anafanya shuguli zake binasi.
Moja kati ya kitu kilichofanya harusi ya Prof. Kapuya ichukue headlines mtandaoni kutokana yeye kuwa na umri wa Miaka 74 na mke wake aliyemuoa kudaiwa kuwa na umri wa Miata 25 wakiwa wametofautiana Miaka takribani 49.
LIVE: WEMA SEPETU AITWA TENA NA BODI YA FILAMU