Kwa mujibu wa mtandao wa ‘The Guardian’ unaeleza kuwa vituo 23 vya radio nchini Canada vimeacha kupiga nyimbo zote za Mfalme wa Pop Marehemu Michael Jackson kutokana na makala ya ‘Leaving Neverland’ ambayo ilionyesha mashuhuda waliofanyiwa vitendo vya ulawiti na mfalme huyo.
Inaelezwa kuwa kituo cha RNZ kutokea nchini New Zealand ndicho kituo cha kwanza kufikia maamuzi hayo huku wafanyakazi wake wakidai kuwa wanasikiliza maamuzi yanayofanywa na wasikilizaji wao ambapo inatajwa kuwa idadi ya wasikilizaji hufikia laki sita kwa siku na hivyo maamuzi hayo yametolewa na wasikilizaji na kudai kuwa hawawezi kusikiliza nyimbo za mbakaji.
Kupitia vyombo vya habari mbalimbali nchini New Zealand na Canada vinaeleza kuwa vitapiga nyimbo ambazo wasikilizaji wanazitaka na kueleza kuwa hawajajua itachukua muda gani mpaka kuja kurudisha nyimbo za Mfalme huyo katika vyombo vya habari.
VIDEO: MAISHA YA SOUDY BROWN BILA BOSS RUGE “HAKUTAKA TUFANYE UMBEA TU”