Kupitia mtandao wa Elle uliripoti kuwa mwimbaji Justin Bieber alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya akili (Mental Health) miezi kadhaa iliyopita na sasa mwimbaji huyo ameweka wazi kuwa anapitia wakati mgumu kiafya.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Justin Bieber ameweka wazi kuhusu maendeleo yake ya kiafya na kudai kuwa anapitia wakati mgumu na anahitaji maombi kutoka kwa mashabiki ili afya yake iweze kuimarika zaidi kutokana nan yeye kupitia magumu.
“Nilitaka kuwapa taarifa juu ya maendeleo kwa kile ninachokipitia, nimekuwa nikipitia magumu, najiskia tofauti, huwa narudi nyuma na siogopi nilitaka tu niwafikie na kuwaomba mniombee. Mungu ni mwaminifu na maombi yenu yanafanya kweli kazi nashukuru, kwenye msimu wa binadamu nimekuwa nikitazama vitu vyangu kichwa juu” >>>Justin Bieber
VIDEO: Irene Uwoya kaamua kuweka wazi siri za urembo wa ngozi yake