Habari za Mastaa

ROSTAM wamezikana nyimbo mbili zinazosambaa mtandaoni “Sio sisi”

on

Baada ya kusambaa taarifa kuhusu nyimbo zinazodaiwa kuwa ni za Roma na Stamina (Rostam) mmoja ukiwa na maudhui yanayomchana msanii Dudu Baya na mwingine ukiwa na maudhui, hatimaye ROSTAM wametoa ufafanuzi kuhusu hilo kwa kuandika haya.. 

“Tukiwa Kwenye Kipindi Hiki Kigumu Na Nyakati Za Mashaka/Hofu Na Simanzi Kama Hizi, Kwa Kuondokewa Na Wapendwa Wetu Duniani Hapa Tunapenda Kuchukua Nafasi Hii Kuwapa Pole Ndugu Jamaa Na Marafiki Wote Wanaoguswa Kama Sisi Na Misiba Hii!!

“Sambamba Na Hayo Tunapenda Kuutangazie Umma Ya Kuwa Kuna Habari Zinazoendelea Hasa Katika Mitandao Ya Kijamii Na Radio Mbali Mbali Ya Kuwa Kunazo Nyimbo Kadhaa Zinatoka Na Zinaandikwa Kuwa Walioimba Ni #ROSTAM Yaani #ROMA #STAMINA Wakishirikiana Na Wasanii Wengine!! Habari Hizi Hazina Ukweli #Hizo_Sauti_Na_Uandishi Sio Wa #Roma Wala #Stamina”

“Tumekuwa Tukiulizwa Sana Na Vyombo Vya Habari Kuhusu Hilo Na Tumeona Ni Vema Tukawataarifu Kwa Pamoja Katika Ukurasa Huu Kuhusiana Na Habari Hizo!! Tunayasema Haya Kwa Sababu Inawezekana Wanaosema Ni Sisi Wanafurahishwa Na Kile Kilichoimbwa Katika Ngoma Hiyo/Ngoma Hizo

Lakini Mtu Huyo Huyo Aliyeimba Siku Akija Kuimba Akamtukana Mama Yako Au Baba Yako Sidhani Kama Kitakufurahisha Pia!! Na Utawachukia #ROSTAM Ukiamini Wao Ndio Wenye Sauti Hizo!! hivyo Ni Vema Tutambue Ya Kuwa Hao Mnaowasikia Sio #Rostam Kwa Kumalizia tu Wimbo Wa Mwisho Wa #Roma Kuutoa Ilikuwa Ni #ZIMBABWE na Wimbo wa Mwisho Wa #Stamina Kuutoa ilikuwa ni #LoveMe na Wimbo wa Mwisho Wa Kundi #Rostam Kuutoa Ilikuwa Ni #Kaolewa Baada Ya Hapo Hakuna Kazi Binafsi Zilizotoka Tena!!

PART 2: ROMA KAFUNGUKA RUGE ALIVYOIPAMBANIA ‘PARAPANDA’

Soma na hizi

Tupia Comments