Beki wa zamani wa club ya Man United na Juventus Patrice Evra ameonesha chat kati yake na Cristiano Ronaldo walizokuwa wanawasiliana kabla na baada ya game ya Juventus dhidi Atletico Madrid ambapo katika chat hizo Evra alikuwa akimuhamasisha Ronaldo kuwa anamtegemea sana katika game hiyo kitu ambacho alikitekeleza katika mchezo wa marudiano dhidi ya Atletico Madrid.
Katika mchezo huo Ronaldo alifunga hat-trick katika ushindi wa 3-0 agg 3-2 na kutinga robo fainali “Nyuma ya pazia hizi ni meseji kati yangu na Cristiano Ronaldo siku tano kabla ya game (vs Atletico Madrid), hii ni kuonesha kuwa kulikuwa na hali gani ya kujiamini na sehemu ambapo unatarajia kufika kutoka kwa mchezaji bora duniani”>>> Evra
Patrice Evra na Cristiano Ronaldo ukaribu wao mkubwa ulianzia walipokuwa wanacheza pamoja katika club ya Man United, Ronaldo alikuwa Man United katika kipindi cha miaka sita (2003-2009) wakati Evra nae alikuwa Man United katika kipindi cha miaka nane (2006-2014), hivyo Evra na Ronaldo wamecheza timu moja kwa miaka mitatu wakiwa pamoja.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke