Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

The Game amkingia kifua Michael Jackson ni kuhusu skendo ya ulawiti

on

Mfalme wa Pop Marehemu Michael Jackson ameonekana kupata mtetezi juu ya skendo ya ulawiti inayoendelea. Hivyo Rapper The Game ametumia ukurasa wake wa instagram kumkingia kifua Michael Jackson na kusema kuwa tumuache mfalme apumzike.

The Game ametengeneza cover yenye sura ya MJ na kuandika ujumbe unaomtetea MJ kisha kuuanika kuupitia ukurasa wa instagram ambapo ujumbe wa cover hiyo unasema “Ukweli haudanganyi, watu hufanya” kwenye caption akaandika kuwa MJ hana hatia inatupasa tumuache mfalme apumzike.

Michael Jackson anakabiliwa na tuhuma za ulawiti toka kwa wanaume kadhaa ambao walithibitisha kufanyiwa vitendo hivyo wakiwa na umri mdogo.kupitia makala fupi ya ‘Leaving Neverland’ iliyorushwa na mtandao wa TV ya HBO .

VIDEO: KIJANA ALIEFELI MASOMO, ANAYO CARWASH INAYOTEMBEA, KAJENGA NYUMBA

Soma na hizi

Tupia Comments