Club ya Mbao FC ya jijini Mwanza leo imetangaza rasmi kumteua aliyekuwa kocha mkuu wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Salum Mayanga, kuwa ndio kocha wao mpya mkuu, Mbao FC limemtangaza Mayanga kama mrithi wa Ally Bushiri.
Salum Mayanga anaichukua timu kutoka kwa kocha Ally Bushiri aliyefutwa kazi katika timu hiyo akidumu kwa miezi minne tu, toka achukue mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Amri Said aliyejiuzulu kwa kupinga kuletewa Ally Bushiri kama msaidizi wake wakiwa wana kiwango sawa cha elimu ya ukocha.
Baada ya Mbao FC kuachana na kocha wake Amri Said December 19 2018 kutokana na kutopenda kuletewa Ally Bushiri kama msaidizi wake kwa madai wana elimu sawa, walipaswa kumletea aliyejuu yake awe mkuu wake au aliyechini yake kielimu ili awe msaidizi wake, timu hiyo imeishia kushuka kwa nafasi 11 toka imeanza kuwa chini ya Ally Bushiri.
Hadi anaondoka Amri Said Mbao FC ilikuwa nafasi ya 4 katika msimamo wa TPL tofauti na sasa ipo nafasi ya 15, Mbao FC chini ya Amri Said akiwa kaifundisha Mbao FC katika game 17 za TPL, ameshinda game 6, amefungwa game 5 na ametoka sare game 6, akifunga magoli 12 na kuruhusu kufungwa magoli 16 timu ikiwa nafasi ya 4 kwa kuwa na point 24.
Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!