Habari za Mastaa

Album ya Jay Z ‘The Blueprint’ imeingizwa makumbusho ya Taifa Marekani

on

Album ya sita ya Rapper Jay-Z ‘The Blueprint’ imeweka historia kwa kuingizwa kwenye makumbusho ya taifa (Library of Congress or National Recording Registry) eneo ambalo huhifadhiwa kazi bora za wasanii zilizoegemea upande wa utamaduni, ubora wa mpangilio na historia.

Album ya The Blueprint iliyotoka September 11, 2001 inatajwa kuwa miongoni mwa album zilizowahi kufanya vizuri kwa muda wote duniani. Album hiyo imeungana na Albums kibao ikiwemo ‘Love Supreme’ ya John Coltrane, ‘Ok Computer’ ya Radiohead na ‘Straight Outta Compton’ ya NWA.

Inaelezwa kuwa Album hiyo iliachiwa rasmi sawa na siku ambayo Marekani ilipata shambulio la kigaidi ‘September 11’ na kusababisha vifo vya maelfu ya wananchi wa Marekani katika jengo la “Twin Towers” .

 

VIDEO: BIFU!! AMBER LULU NA HAITHAM WATIBUANA, ADAIWA KUIBA MUME

Soma na hizi

Tupia Comments