Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe leo March 26, 2019 amezungumza na Waandishi wa Habari juu ya kinachoendelea baina yao na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa alietangaza kutaka kukifuta Chama hicho.
Nimekusogezea mambo kumi na tano aliyozungumza Zitto Kabwe na Waandishi wa Habari katika Ofisi za ACT Wazalendo.
”Tunajua wanaogopa kuwa hawatashinda uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2020 na kuna mtu wanamuogopa lakini yule ni mtanzania kama watanzania wengine’ Zitto Kabwe#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/ZF6iN1e2pl
— millardayo (@millardayo) March 26, 2019
“Msajili wa Vyama vya Siasa anasema katika mkutano wetu wanachama walitumia maneno yenye kuhamasisha udini. ACT ni Chama Cha Kisiasa ambacho kimesajiliwa kwa kufuata misingi ya Kikatiba na wala si kwa misingi ya udini wa ukabila” Zitto Kabwe#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/vBR5iP0xJA
— millardayo (@millardayo) March 26, 2019
“Tutamjibu Msajili wa Vyama na vithibitisho vyote” Zitto Kabwe#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/vLXjdCHcPH
— millardayo (@millardayo) March 26, 2019
“Msajili amejipa kazi ya kutoa tafsiri ya maneno ya Dini ya Kiislamu ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa hakuna kadhi, basi hili tumpe kazi Mufti atoe fwataa juu ya matumizi ya maneno ya Kiislamu yasitumike katika mikutano ya kisiasa” Zitto Kabwe#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/hn6Hgau95V
— millardayo (@millardayo) March 26, 2019
“Tunajua hofu iliyopo kwa @ACTwazalendo, wajue kuwa Maalim Seif ni mtanzania kama mtanzania mwingine yoyote, wamemnyang’anya ushindi mara 5, wamemfukuza uanachama, wamemnyamg’anya chama, wamemfunga, lakini bado hawachoki” Zitto Kabwe#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/923mjSiqxb
— millardayo (@millardayo) March 26, 2019
“Namshauri Msajili wa Vyama vya Siasa afanye mambo anayoyajua na aache mambo asiyoyajua kwa wenye uelewa wa mambo hayo” Zitto Kabwe#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/gNTSmiqMnT
— millardayo (@millardayo) March 26, 2019
“Msajili anatuhumu kuwa Wanachama wa ACT Wazalendo kuwa wamechoma bendera za CUF jambo ambalo hana uhakika nalo sababu hana uhakika kama wale ni wanachama wa ACT Wazalendo hata Mahakamani hawezi kuthibitisha” Zitto Kabwe#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/jOTYY4dZfI
— millardayo (@millardayo) March 26, 2019
“Inashangaza Msajili anatuandikia barua ya kututisha kutufutia Chama chetu, ilipaswa ajiridhishe kama kweli hao walikua ni Wanachama wetu kwa sababu sisi watu wetu tunawajua” Zitto Kabwe#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/yXHA3D2UwS
— millardayo (@millardayo) March 26, 2019
“Mimi nafahamu Msajili si Mhasibu wala si Mkaguzi na sijui ofisini kwake kabla ya kutuandikia barua aliyotuandikia alishauriana na Wahasibu wa ofisini kwake, sina hakika kabla ya kutuandikia barua aliwasiliana na Mkaguzi wa Hesabu” Zitto Kabwe#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/w55N6wKJF2
— millardayo (@millardayo) March 26, 2019
”Kazi ya Chama ni kuwasilisha hesabu kwa CAG sio Chama kukagua hesabu zake chenyewe, kisha CAG anakagua na anakiletea chama ripoti kisha chama kinampelekea Msajili wa Vyama ripoti hiyo na hakuna mwaka hatujafanya hivyo” Zitto kabwe#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/XjlWE5GvMP
— millardayo (@millardayo) March 26, 2019
”Tangu CAG aanze kukagua vyama, ACT Wazalendo ndio chama cha kwanza cha siasa nchini kupata hati safi” Zitto Kabwe#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/mIhs90GwmK
— millardayo (@millardayo) March 26, 2019
“Sisi kama ACT Wazalendo tumefanyiwa ukaguzi wa mahesabu yetu katika barua ambayo ameiquote Msajili wa Vyama vya Siasa na kupata hati safi yaani Unqualified Audit Report, na ACT Wazalendo ndiyo Chama Cha kwanza kupata hati safi hapa nchini” Zitto Kabwe#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/Clc8hk6bwf

LIVE: ZITTO KABWE AJIBU ISHU YA MSAJILI KUTAKA KUKIFUTA CHAMA CHA ACT WAZALENDO