Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ameeleza msimamo wake kuhusiana na Shomari Kapombe ambaye aliumia mwaka jana akiwa katika majukumu ya Taifa Stars, RC Paul Makonda ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji ya Taifa Stars aliahidi Tsh milioni 10 kwa kila mchezaji kama wataiwezesha Taifa Stars kufuzu AFCON 2019.
Sasa baada ya zawadi hiyo kutoka na wachezaji kupewa viwanja na Rais Magufuli kama sehemu ya zawadi kwa kuiwezesha Taifa Stars kufuzu AFCON 2019 kwa kuifunga Uganda 3-0, Samatta ameamua kuwakumbusha shirikisho la soka Tanzania TFF kuwa Shomari Kapombe anatakiwa kukumbukwa katika mgao huo.
“Shomari kapombe kama captain ningeomba TFF imuangalie katika zawadi ambazo wachezaji watapata, ikishindikana basi ningeomba wachezaji wote tumchangie kidogo kidogo na endapo vyote visipowezekana kabisa basi katika ahadi ya Mh Paul makonda, nitagawana nae nusu kwa nusu”>>> Samatta
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Shomari Kapombe aliumia mwishoni mwa mwaka jana akiwa na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars katika mazoezi ya mwisho Afrika Kusini kuelekea Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza AFCON 2019, toka ameumia Kapombe hajarudi uwanjani rasmi hadi Taifa Stars inacheza na Uganda.
MUHIMBILI JKCI NAO WATANGAZA NUSU BEI KWA USHINDI WA TAIFA STARS