Tukiwa tunaelekea kumaliza msimu huku ikiripotiwa kuwa kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer hayupo sawa na kiungo wake Paul Pogba kutokana na kiungo huyo kuonesha dhamira ya dhati ya kutaka kuihama club hiyo na kujiunga na Rea Madrid ya Hispinia mwisho wa msimu, leo zimeripotiwa taarifa mpya kuhusiana na tetesi hizo za Pogba kwenda Real Madrid.
Kutoka mtandao wa dailymail.co.uk ya England umeripoti kuwa uongozi wa juu wa Man United umeamua kutoa masharti yake juu ya Pogba, Man United wamemwambia wakala wa Paul Pogba anayejulikana kwa jina la Mino Raiola kuwa kama Real Madrid wanamtaka mchezaji huyo basi wailipe Man United walaum kuanzia Pound milioni 130 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 390 ili wampate.
Kiasi walichotaja Man United kinaashiria kama ni mbinu za kuitaka Real Madrid ishindwe kufanikisha hilo, kwani pamoja na tetesi zote na kudai Pogba kutaka kuondoka wanajipanga kumpa mkataba mnono utakomfanya alipwe pesa ndefu, inaelezwa kuwa baada ya Zidane kurudi Real Madrid atauza wachezaji wengi sana ili ajenge upya kikosi chake.
Mwana FA kakutana na Jose Mourinho uso kwa uso, kamwambia yale maneno yake?