Leo Aprili 16, 2019 Serikali imefanya ubinafsishaji wa viwanda 176, huku ikivifuta viwanda 20 kwenye orodha ya viwanda nchini pamoja na kuvirejesha serikalini viwanda 15 ili kuvitafutia wawekezaji wengine.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda amesema zoezi la ubinafsishaji limefanyika vizuri na viwanda 20 vimefutwa kutokana na makosa ya kuuza mali moja moja na kuvifanya visiendelee.
Miongoni mwa viwanda 20 vilivyofutwa kipo cha Gypsum, Kiwanda cha Liquid, Kiwanda cha TANCUT Almas, TDL Mbeya, Kiwanda cha Matrla ya Malori, Arusha Metal na Kiwanda cha Nyama cha Tanganyika Packers.
“Vimefutwa kwa sababu vimekosa sifa viliuza mali moja moja hivyo ni kosa, pia tumevirejesha viwanda 15 serikalini ili kutafuta wawekezaji wengine,“amesema.