Mwigizaji Elizabeth Michael ametimba kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM leo April 16,2019 ambapo amefunguka vitu vingi kupitia mahojiano aliyoyafanya ikiwa na kugusia ishu iliyosambaa miezi kadhaa iliyopita kuhusu kumuwekea limbwata mume wake mtajarijiwa Majizzo kupitia mitandao ya kijamii.
Elizabeth Michael amefunguka pia kuhusu kurudi kwenye industry ya filamu hivi karibuni baada ya mashabiki kuuliza sana swali hilo, hivi ndivyo baadhi ya vitu ambavyo Lulu amevizungumza leo kwenye kipindi cha XXL .
“Kiukweli kwenye tasnia ya filamu tumeyumba kwa kiasi fulani na hata ukiangalia uzalishaji wa filamu umepungua sasa kama uzalishaji umepungua hata ushirikishwaji wa tuzo za filamu kwa nchi zingine umepungua, Tupo kwenye wakati wa kuboresha tasnia yetu hivyo nina imani mambo yatakuwa sawa mbeleni”
“Mimi na mwenza wangu Majizzo bado hatujaoana. Sisi tabia zetu zinaendana ni watu wa kawaida hivyo tutafunga ndoa kawaida yaani ndugu upande wa kiume na upande wa kike pamoja na marafiki zetu baadhi. Baby wangu sio tajiri bali ni mtu ambaye ameanzia chini kimaisha mpaka kufika alipofika na am proud kwa hilo”
“Story ambazo zilikuwa zinasambaa mitandaoni kuwa nimemuwekea ‘Limbwata’ mpenzi wangu, niliziona kwenye mitandao ya kijamii kama wengine walivyoziona na kiukweli hazikuniumiza kabisa maana mwanzoni zilikuwa zinanipa shida sababu nilikuwa nazifatilia lakini kwa sasa sizipi nafasi ya kuzifatilia maana kitu unavyokipa nafasi ndivyo kitakavyo kuumiza”
“Kwenye movie nitarudi hivi karibuni, nahitaji kukua sehemu zote, sio tu kwenye maisha yangu bali hata kwenye kazi zangu na vitu vingine, nipo kwenye process ya kurudi kwenye movies na itachukua muda kurudi kwa sababu nataka utofauti na vile nilivyokuwa navifanya zamani kwenye movies”
VIDEO: SEVEN MOSHA AWEKA WAZI AKAUNTI YA MKE WA ALIKIBA INSTAGRAM