Inaripotiwa kuwa baada ya Rapper Kodak Black kuahirisha kufanya show siku ya April 17,2019 mjini Boston Marekani kitendo hicho kimewafanya mashabiki zake kukasirika na kujikusanya katika gari lake la ziara mpaka kufikia hatua ya polisi kuingilia kati baada ya kuonekana kuanzishwa kwa vurugu.
Imeripotiwa kuwa Kodak Black alitarajiwa kutumbuiza kwenye show hiyo ambayo ilipata mahudhurio mazuri lakini hakutokea kwenye ukumbi huo kiasi cha kusababisha vurugu kwa mashabiki ambao walikuwa tayari wamelipa pesa na kuingia ukumbini, uongozi wake bado haujatoa sababu ya rapper huyo mtata kuahirisha show.
Inadaiwa kuwa kutohudhuria show hiyo wengi wametoa mawazo yao na kusema kuwa huenda Kodak aliogopa wingi wa watu waliojitokeza na kuhisi kuwa angepigwa au kujeruhiwa kutokana na kauli aliyoitoa kuhusu mke wa Marehemu Nipsey aliposema anamtani.
AUDIO: Ulipitwa na hii ya mwigizaji Irene Uwoya kutema cheche “Kuna watu nikuwafungia vioo tu”? Bonyeza PLAY hapa chini kusikiliza.