Leo April 29,2019 Vanessa Mdee amekutana na nguli wa muziki Barani Afrika M’bilia Bel mwenye umri wa miaka 58. Mbilia Bel ni raia wa Congo na anasifika kwa sauti yake nzuri na anamiliki ngoma kibao ikiwemo Nakei Nairobi ambayo ilimpatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya Afrika, Nadina na nyingine nyingi.
Vanessa Mdee ameonyesha furaha yake kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya kukutana na mkongwe huyo akiwa bado nchini Congo kwa ajili ya kazi zake za muziki ambapo pia amedokeza juu ya ujio wa ngoma yake mpya pamoja na mkali wa muziki wa dansi Fally Ipupa ambayo itakuja hivi karibuni.
“My team organized the best surprise. If you know me you know I STAN A QUEEN 👑 Leo nimekutana na Malkia wa mziki wa Congo na Afrika Mbilia Bel @mbilia_belFAN GIRL MOMENT. Sipati picha ni jinsi gani amepambana, nampenda sana ORIGINAL AFRIKAN POP QUEEN 👑” >>>Vanessa Mdee
Nikukumbushe M’bilia Bel ambaye anajulikana kama malkia wa Congo na muziki wa Rumba barani Afrika, kipaji chake Mbilia Bel kiligunduliwa na Sam Manguana na baadae Tabu Ley Rochereau akamsaidia sana katika muziki katika suala zima la kujiamini na kuanza kufanya poa.
Miaka ya 1980 ndio nyota ya Mbilia Bel liana kung’a baada ya kujiunga katika band ya Tabu Ley, Marsha ya muziki yalizidi kung’aa zaidi 1988 alipohamia Paris Ufaransa na kuanza kufanya kazi na mpiga guitar Bamundele na kati ya mwaka 1989 hadi 1990 alibahati kufanya ziara kubwa ya kimuziki katika nchi za Ulaya, USA na Afrika Magharibi.
VIDEO: BALAA LA NANDY WAKATI AKIIMBA WIMBO WA NINOGESHE NAIROBI