Mwimbaji kutokea kwenye industry ya Bongo Fleva Tunda Man ameweka wazi kuhusiana na taarifa za kifo chake zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupata ajali siku ya Pasaka na kusema kuwa ni kweli alipata ajali lakini sio kama inavyoonekana kwenye picha.
Kupitia mitandao ya kijamii picha mbalimbali zimekuwa zikisambaa zikionyesha tukio la ajali mbaya lilitokea Arusha siku kadhaa zilizopita na kulihusisha na ajali ya Tunda Man na huku taarifa zingine zikiripoti kuwa amefariki dunia.
Tunda Man ameomba radhi kwa ndugu jamaa na marafiki waliopokea taarifa hizo na anamshukuru Mungu kutokana na ajali hiyo aliyoipata hakuna hata mmoja aliyepata madhara pia anawapa pole wale wote waliokutwa na msiba kwenye picha ambayo imetumika kusambaa kwa taarifa ya kifo chake.
“Nilipopigiwa simu ya kwanza nilihisi labda ni kawaida mana waandishi wa kibongo nimewazoea kila siku kuoanisha mambo lakini siku zinavyosogea naona habari inanizidia ni kweli nilipata ajali lakn sjaelewa ni nani katengeneza hyo picha kweli nilipata ajali ila sio kwnye hiyo picha, na pili mimi ni mzima wa afya kabisa ila nasikitika kwa wale ambao bado wanaendelea kuedit picha za matukio tofauti na kujumuisha na ajali niliyoipata siku ya pasaka”
“Huyo sio mimi naomba nieleweke hvyo,Pia naomba radhi kwa ndugu jamaa na marafiki ambao pia walipokea taarifa kama hizi, lakini nashukuru mungu katika ajali tulisalimika wote bila madhara yyte ila sio ajali hyo.Pia niwape pole kwa wote walokutwa na msiba huo kwnye picha hiyo ,Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi .Amen🙏”
VIDEO: ULIPITWA NA HII KULA NA VIJITI NAPO KIPAJI, OMMY DIMPOZ KACHEMKA “SIPENDI UJINGA”? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO