Kwa mujibu wa mtandao wa ‘The Blast’ umeripoti kuwa kesi zinazomkabili mwimbaji R.Kelly zitaanza kusikilizwa hivi karibuni mjini Chicago ambapo mpaka sasa kesi zinazomuandama ni unyanyasaji wa kingono, ukwepaji kodi ikiwemo na kusafirisha wanawake kwa ajili ya kufanya nao ngono.
Inaelezwa kuwa mwanasheria Raed Shalabi ambaye amezungumza na mtandao huo wa The Blast amesema kuwa R. Kelly amekuwa na mawazo tofauti kuhusiana na kesi zake na anaamini kuwa Mahakama ya Chicago itafanya vitu kwa usawa mkubwa na sheria zitafanyika ili jina lake lisafishwe. Raed Shalabi ni mwanasheria mpya ambaye ameongezwa ili kutetea kesi ya Kelly.
Shalabi aliongozea na kusema kuwa anaamini kesi iliyofunguliwa na Heather Williams dhidi ya R.Kelly ni lengo la kujipatia kipato hajawahi kuona mwathirika wa kesi flani anafunguliwa mashtaka na kudai pesa hivyo watu wote waliopo kinyume na R.Kelly wanahitaji pesa.
Shalabi ameweka wazi kuwa kwa sasa R. Kelly anataka kuweka kila kitu nyuma na kuzingatia kuhusu kazi zake za muziki ila kwa sasa Kelly hana tamasha lolote la kufanya lakini malengo yake ni kurudi kwa kasi kwenye steji.
VIDEO: NANDY AONYESHA STUDIO YAKE ALIYOJENGA NYUMBANI, KAONGELEA SHOW YA SUMBAWANGA NA MTOTO WA RUGE