Wanunuzi wa mbegu za Alizeti wamelalamikia uwepo wa vibali na tozo nyingi wakati wa ununuzi na usafarishaji wa mbegu za zao hilo hali inayotajwa kuchangia baadhi yao kukata tamaa kwa kugeukia biashara nyingine huku wengine wakilazimika kwenda kununua nchi jirani ya Malawi.
Kutokana na changamoto hizo baadhi ya wanunuzi hao hususani Wanawake wameeleza wanalazimika kutoa rushwa ya ngono kwa baadhi ya mawakala ili kusafirisha bidhaa hiyo kwa urahisi kwa lengo la kukwepa vikwazo ambavyo vimekuwepo.
Martin Mgallah ni Meneja was zao la Alizeti wa Programu ya kuendeleza mifumo ya kimasoko katika Kilimo (AMDT) anasema kutambua changamoto zinazowakabili wakulima nchini AMDT imedhamiria kuwaunganisha wakulima wa Alizeti na wadau wote muhimu katika mnyororo wa thamani wa zao hilo.
NAIBU WAZIRI APIGA MAGOTI AKIOMBA BARABARA “ITACHACHA NA HAITALIKA HAWATANIELEWA”