Top Stories

Siku 14 za Shamim na mumewe gerezani, upelelezi kesi yao haujakamilika (+video)

on

Leo Mei 27, 2019 zimetimia siku 14 kwa mmiliki wa Blog 8020 Fashion, Shamim Mwasha (41) na mumewe, Abdul Nsembo(45) gerezani huku upelelezi wa kesi yao ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride bado haujakamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazi, Kelvin Mhina kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika, hivyo anaomba ahirisho.

Baada ya kueleza hayo Wakili utetezi, Charles Kisoka amedai kuwa shauri hilo halina dhamana hivyo wanauonba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.

Wakili Wankyo ameeleza kuwa amesikia kilichozunguzwa na upande wa utetezi, hivyo watawahimiza wenzao wa upelelezi wafanye haraka na tarehe ijayo wataeleza upelelezi ulipofikia.

Hakimu Kelvin Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi June 10, 2019, washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu kesi yao haina dhamana.

Washtakiwa hao wanatuhumiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya, Mei 1,2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini  Dar es Salaam kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.

“HALI NI MBAYA NI KINYAA WANAFUNZI WANAJISAIDIA NJE” MWALIMU AKIPOKEA MSAADA TOKA KWA MWASELELA

Soma na hizi

Tupia Comments