Tunayo stori kutokea kwa Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC Dar es salaam, Anthony Lusekelo ambapo amefunguka na kusema kuwa angekuwa Waziri Mkuu angemshauri Rais afute Uchaguzi wa Serikali za Mtaa kwa sababu ni gharama.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mchungaji Lusekelo amesema waliopo madarakani waendelee na nafasi zao, hivyo anaomba uchaguzi wa Serikali za Mtaa ufutwe ili kutoisumbua nchi.