Raisi wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon anaamini Cristiano Ronaldo anaweza kurudi Manchester United huko mbeleni.
Mshambuliaji huyo wa Ureno alitumia miaka 6 kuitumikia klabu ya Old Trafford kati ya mwaka 2003 na 2009 kabla ya kuhamia Madrid kwa ada ya uhamisho iliyoweka rekodi wakati huo ya £80 million.
Ronaldo ambaye mpaka sasa ameshafunga magoli 41 katika mashindano yote msimu huu ambapo alikuwa akihusishwa na kurejea katika klabu yake ya zamani kabla ya kusaini mkataba mpya na Madrid, lakini Calderon anaamini mchezaji huyo anaweza kurudi kuvaa jezi nyekundu huko mbeleni.
“Huwezi kujua,” aliiambia talkSPORT. “namfahamu, mimi ndiye niliyemsaini, alikuwa akisema kwamba Manchester ni kama nyumbani kwake, alikuwa na furaha sana pale pamoja na mshabiki’
“Kwa wakati ule na Ferguson, alikuwa akimuona kama baba yake, na kila kitu ndani ya Manchester kilikuwa kizuri lakini alihitaji changamoto mpya na akaamua kuja kuichezea Real lakini huwezi kujua, labda mwishoni anaweza kurudi England kule Manchester kumalizia soka lake.”