Michezo

Alichosema Uhuru Selemani kuhusu kubaki au kuondoka Simba msimu ujao.

on

Screen Shot 2014-03-22 at 12.21.44 PMWinga wa timu ya Simba ya Dar es Salaam Uhuru Selemani ambae alirudi kwenye klabu hiyo mwaka jana akitokea Coastal Union amefunguka juu ya mustakabali wake ndani ya klabu hiyo.

Uhuru ambae amekuwa akiwekwa benchi na kocha Zdracko Logarusic, amesema ikiwa anahitaji kuendelea kucheza soka basi kwa sasa klabu ya Simba haimfai kwa sababu anakosa nafasi hivyo ni bora ahame na kwenda kutafuta klabu nyingine.
UhuruSeleman1
Amezungumza na gazeti la Mwanaspoti na kusema “nikikubali kubaki Simba naamini nitaua soka langu, hata kama wakinihitaji nibaki kwa kweli sibaki. sasa nafikiria kuchezea timu nyingine tofauti na Simba kwani zipo nyingi zinazoweza kunisajili, maisha popote na hilo linawezekana kutokana na kiwango changu, nikimaliza mkataba wangu naondoka.”

Tupia Comments