Hiki ndio kipindi cha usajili wa wachezaji soka duniani kote, wakati vilabu vikihaha kuhakikisha vinanasa saini za wachezaji wapya, zipo timu pia zinapambana kuhakikisha zinawabakisha wachezaji wao waliopo katika vikosi vyao, kwa sasa kuna tetesi kuwa Ibrahim Ajib wa Yanga anaondoka timu hiyo.
Ibrahim Ajib alijiunga na Yanga akitokea Simba SC kwa mkataba wa miaka miwili misimu miwili iliyopita, hivyo kwa sasa mkataba wake umemalizika Yanga, mwisho wa mwezi huu atakuwa mchezaji huru ila inaonekana Yanga hawajaafikiana na mchezaji huyo na tetesi za kuhusishwa kurudi Simba SC zinaweza kuwa na ukweli.
Dalili kuu iliyodhihirisha hilo ni kitendo kilichotokea wakati wa kumtambulisha mchezaji mpya wa Yanga kutokea Police FC ya Uganda Balinya Juma kuonekana akitambulishwa akiwa na jezi namba 10 wakati wa hafla ya uchangiaji Yanga June 15 ukumbi wa Diamond Jubilee, jezi ambayo huvaliwa na Ibrahim Ajib, hivyo ni nadra kumtambulisha mchezaji kwa jezi yenye namba ambayo tayari ina mchezaji anaitumia
EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega