Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza kupitia Jeshi hilo limeiomba Serikali kuwalipa deni la shilingi Bilioni 6.45 fedha zilizotumika katika uzabuni pamoja na huduma za chakula kwa Wafungwa na Mahabausu hali iliyosababisha Shirika kushindwa kutekeleza shughuli za kimaendeleo.
Hayo yameelezwa Mkoani Morogoro na Kamishina Jenerali wa Magereza nchini CGP Faustini Kasike katika kikao cha bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi cha Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza kwa mwaka wa fedha 2019-2020 ambapo ameeleza baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwemo ufinyu wa fedha kutokana na deni hilo huku Mkurugenzi wa Shirika hilo akielezea mikakati waliyojiwekea baada ya bajeti hiyo.
KAMANDA KAZUNGUMZA KUHUSU MWALIMU MKUU ALYEMPA WANAFUNZI WAKE UJAUZITO “ALIACHIWA”