Mzazi mwenza na staa maarufu kutokea Nigeria Wizkid ambaye pia ni Meneja wake Jada Pollock ametoa siri kubwa kupitia insta story yake na kusema kuwa ameamua kujitoa na kutosimamia tena kazi za msanii huyo na amekuwa kwenye mahusiano yenye manyanyaso.
Jada alienda mbali na kutoa malalamiko juu ya msanii huyo na kudai kuwa amekua akipigwa kwa miaka mingi sasa lakini alifanya tukio hilo kama siri mbele ya marafiki zake pamoja na ndugu na kuisha pamoja na Wizkid kumemfanya kuhisi nyumba hiyo kama sehemu ya mashambulio na amejitahidi kufanya marekebisho ili kila kitu kiwe sawa lakini anambidi aachie ngazi.
“Kuanzia leo Ayo na mimi hatutofanya kazi pamoja nimekuwa kwenye mahusiano yenye manyanyaso kwa miaka sasa na nimemvumilia kwa sasa nimechoka, Wiz Kid amekua akinipiga na kuniacha na makovu lakini nimelificha hili kwa dunia nzima nikijumuisha marafiki zangu pamoja na familia”
“Inanifanya nijisikie tunaishi kwenye nyumba yenye mashambulio, nimefanya kila niwezalo ili kutatua lakini kuanzia leo naliachia, unawezakumpa mtu msaada kadri uwezavyo lakini inafikia wakati inabidi ujithamini, siwezi kumlea mwanangu kwenye mazingira dhaifu” >>> aliandika Jada Pollock
Superstar huyo ana jumla ya watoto watatu wa kiume ambao amezaa na wanawake watatu tofauti akiwemo Jada Pollock ambae amezaa nae mtoto wake wa tatu Zion hata hivyo mwanamke aliyezaa na Wizkid mtoto wa pili Binta Diamond Diallo aliwahi pia kutoa malalamiko kuwa Wizkid hatekelezi wajibu wake kama baba kwa mtoto wake hatoi matunzo
VIDEO: UWOYA KAFUNGUKA “NIKO NA MPENZI, NAKULA BATA, NINA NYUMBA MBEZI BEACH”