Baada ya taarifa kuhusu kesi inayoumuandama Asap Rocky kumfikia Rais Donald Trump na kuamua kutoa tamko kuhusu kesi hiyo na kuahadi kuongea na Waziri Mkuu wa Sweden ili aingilie kati kesi hiyo na kuitatua mapema na Asap awe huru na kurudi Marekani salama.
Sasa Rais Donald Trump ameonekana kushtushwa na taarifa zilizotolewa jana kuhusu rapper huyo kuwa ameshtakiwa kwa kosa la kupigana na kusababisha majeraha na huenda Asap akahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela na ishu hiyo imemfanya Rais Trump kumjia juu Waziri Mkuu Stefan Löfven.
“Nimevunjika sana moyo na matendo ya Waziri Mkuu Stefan Löfven, Sweden imewaangusha wa Marekani Weusi wote nchini Marekani. Nimeutazama mkanda wa ASAP Rocky, na nimeona alikuwa akifuatwa na kusumbuliwa na watu ambao walikuwa wanatafuta matatizo. Tuwatendee haki Wamarekani.” >>>aliandika Rais Donald Trump.
July 25,2019 Mahakama ya Sweden ilimshtaki rapper Asap Rocky kwa kosa la kumpiga na kumuumiza shabiki mmoja katikati ya mji wa Stockholm June 30,2019, hii ni baada ya rapper huyo kusota rumande kwa takribani wiki mbili sasa.
VIDEO: MREMBO ANAEPIGA VITA KUJICHUBUA “UNAWEZA PATA KANSA HATA YA KIZAZI”