Afisa mtendaji mkuu wa Simba SC Mr Magori leo aliongea na waandishi wa habari na kuelezea maandalizi yao ya Simba Day ambayo mwaka huu yatakuwa yanatimiza mwaka wa 10.
“Siku hiyo ya tarehe 31 kingine kitakachofanyika ni kusaini mkataba na mdhamini wa jezi na vifaa vya mazoezi kwa muda ambao tumeingia mkataba wa miaka miwili tuliyokubaliana lakini sherehe yenyewe tutaifanya tarehe 31, jezi rasmi za Simba msimu wa 2019/2020 saa sita usiku tutazionesha kwenye page zetu”>>> Magori
Magori ameeleza kuwa pamoja na kuwa kutakuwa na burudani mbalimbali lakini Simba Day kabla ya kufikia kilele August 6, wachezaji na benchi la ufundi watafanya shughuli mbalimbali za kijamii ila Simba pia itakuwa na wimbo wake maalum ambao utazinduliwa.
VIDEO: Haji Manara hakaukiwi kila siku mpya “Iga Ufe Thisi Is Next Level”