Yanga SC kwa sasa ina mtihani wa kwenda Gaborone Botswana kupindua matokeo ya mchezo kati yao dhidi ya watakaokuwa wenyeji wao Township Rollers, hiyo ni baada ya dakika 90 za game ya Dar es Salaam kumalizika zikiwa na matokeo ya sare ya 1-1 ambayo sio mazuri kwa Yanga ukizingatia wamecheza nyumbani.
Yanga baada ya mwaka 2018 kupoteza 2-1 kwa Township Rollers na kwenda Botswana kulazimishwa sare ya 0-0, tulipata nafasi ya kuongea na moja kati ya wachambuzi mahiri wa soka kwa hapa Tanzania Mwalimu Alex Kashasha na kueleza mtazamo wake kwa namna Yanga walivyocheza wanaweza kusogea hatua inayofuata.
“Kikosi cha Yanga ni kizuri kwa mchezaji mmoja mmoja kule uliona kulikuwa kuna mapungufu katika muunganiko kama timu kutoka kwenye idara ya ulinzi, katikati kwa viungo na mipira kwenda mbele kwenye eneo la ushambuliaji au kwenye eneo la tatu ya mwisho ya kufunga goli, kubwa ninaloliona linalosababisha hiyo hali ni ujio wa wachezaji wengi wapya kwenye kikosi cha Yanga”>>>Kashasha
VIDEO: Yanga yakataa uteja, Sibomana afuta makosa Taifa