Rais Magufuli amekubali ombi la Mkuu wa Mkoa wa DSM Makonda la kupatiwa shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya ya Ubungo Jijini DSM na amemuagiza Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kutafuta fedha hizo ili ujenzi uanze.
“Hatuwezi kuwaacha wananchi wa Ubungo wateseke, wakitaka kutibiwa mpaka waende Wilaya za jirani, hapana, tutajenga Hospitali ya Wilaya ya Ubungo, Ubungo hoyeee” Rais Magufuli.