Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katabi ameingilia kati mgogoro wa mirathi wa watoto wa marehemu Hussein Bakari Dima wanaodaiwa kutaka kudhulumiwa nyumba yao na ndugu wa marehemu baba yao iliyopo eneo la Kizota Area A Dodoma mjini.
Suala hilo ambalo lilianza takribani miezi miwili iyopita ambapo Shangazi Zakhia Said na baba mdogo wao walikuja na hoja ya kutaka kuwakabidhi mali za urithi wa marehemu baba yao kwa kuwa watoto hao wamekwisha kuwa wakubwa na umri Zaidi ya miaka 18 na waweza kujitegemea.
Wakielezea sakata hilo watoto hao Omar Hussein ,29, na Shamila Hussein ,26, walitaka kufahamu mali ambazo shangazi yao anataka kuwakabidhi lakini kinyume na matarajio yao shangazi yao alikuja na watoto wengine wawili akidai ni watoto wa nje ya ndoa wa marehemu ambao wanastahili kugaiwa nyumba hiyo ambayo tangu marehemu baba yao akiwa hai alishawarithisha.
Baada ya kupokea malalamiko ya watoto wa marehemu yaliyofikishwa kwa mkuu wa wilaya ya Dodoma yakionesha kutoridhishwa na uamuzi wa Mahakama ya mwanzo ya Makole iliyotolewa October 28 na hakimu Nduka iliyompa mamlaka shangazi yao Zakhia Said kuwa msimamizi wa mirathi bila wao kusikilizwa watoto hao, mkuu wa wilaya Dodoma Patrobas Katabi amemtaka shangazi huyo kufika ofisini kwake Jumatatu.
VIDEO: BAADA YA KUFUKUZWA AYO TV IMEMFUATA ZAHERA KWAKE “SIJAPEWA BARUA”