Baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa club ya Yanga SC ndio inaonesha zaidi dhamira ya kufanya usajili wa haraka na kutangaza mapema zaidi ukilinganisha baadhi ya timu washindani wao Simba SC na Azam FC ya Chamazi.
Hadi sasa Yanga imesajili wachezaji zaidi ya wawili huku ikisubiriwa kumtangaza rasmi Ditram Nchimbi aliyejiunga nao akitokea Azam FC ila alikuwa kwa mkopo Polisi Tanzania, baada ya tetesi kuwa nyingi Yanga baada ya kumtambulisha Ageyun Ahmad watu walihoji ni kweli Haruna Niyonzima anarudi Yanga kama inavyoripotiwa, afisa habari wa Yanga SC Hassan Bumbuli katoa majibu.
“Nataka niwaambie wana Yanga kuwa zoezi la usajili linafanyika kwa umakini mkubwa sana, tetesi zipo na zitaendelea kuwepo kwa sababu Yanga ni club kubwa na mtu yoyote anayeonekana kufanya vizuri kwenye timu yoyote ile ya nje au hapa Tanzania angependa kuhusishwa na Yanga, kwa hiyo hizo tetesi za akina Haruna Niyonzima na nini ni kwa sababu wanaonekana ni wachezaji bora”>>>Bumbuli
VIDEO: Kauli ya Musonye baada ya Wallace Karia kutangazwa Rais wa CECAFA