Rais wa Marekani, Donald Trump amekuwa Rais wa tatu katika historia ya Marekani kupigiwa kura ya kutumia vibaya Madaraka na Kulizuia Bunge kufanya uchunguzi dhidi yake, hatua hii inampeleka katika kesi dhidi yake itakayoamua kama atabakia Madarakani au laah.
Kipengele cha uchunguzi cha kutumia vibaya Mamlaka kimepitishwa kwa kura 230-197 na kile cha kuzuia utendaji wa Bunge kikapigiwa kura na Wabunge 229 -198, Trump anaungana na Marais wengine wawili ktk historia ya Marekani Andrew Johnson na Bill Clinton,ya kupigiwa kura kama hiyo.
Baraza la wawakilishi lina nguvu ya kumshitaki Rais kwa wingi mdogo wa kura, ila Baraza la Seneti litahitaji wingi wa theluthi mbili kumuondoa Rais Madarakani hatua ambayo sio rahisi kufanyika,kinachosubiriwa sasa ni Baraza la Seneti kuendesha kesi juu ya hatma ya Urais wa Trump.