Msanii mkongwe kutoka nchini Benin Angelique Kidjo mwenye umri wa miaka 59 ameibuka mshindi wa tuzo ya #Grammys kwenye kipengele cha “Best World Music Album” na kumpiga chini Burna Boy ambaye pia alikuwa anawania naye kipengele hicho.
Baada ya ushindi mkongwe huyo alizungumza na kumsifia msanii Burna Boy licha ya kuwa alishindwa kuchukua tuzo hiyo.
“Hii Tuzo na-dedicate Burna Boy, Ni mmoja ya wasanii wadogo ambao wanabadilisha mtazamo wa dunia kuhusiana na Afrika”
Hii inakuwa tuzo ya 4 kushinda Angelique Kidjo ambapo alishawahi kuchukua tuzo hiyo mwaka 2008, 2015, 2016 na mwaka huu 2020.