Ikiwa imepita takribani wiki moja ipite tangu klabu ya Yanga ipoteze mchezo wake dhidi ya Mgambo JKT ya Tanga, leo hii klabu hiyo imewasilisha pingamizi zito dhidi ya mchezaji wa Mgambo na kupinga ushindi wa timu hiyo ya Tanga.
Klabu ya Yanga imewasilisha malalamiko Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa mshambuliaji wa Mgambo Shooting Stars ambaye alicheza dhidi yao katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Mohamed Neto si raia wa Tanzania na hana Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Ingawa malalamiko hayo yamewasilishwa nje ya muda (time barred), TFF imeyapokea na itayawasilisha kwenye Kamati husika kwa ajili ya kupitiwa na baadaye kutolewa uamuzi.
Kwa mujibu wa kanuni, malalamiko yote kuhusu mchezo yanatakiwa kuwasilishwa ndani ya saa 24 baada ya mchezo kumalizika.