Taarifa zilizosambaa leo kutokea nchini Marekani ni kwamba Binti wa Floyd Mayweather, Iyanna (20) huenda akahukumiwa kifungo cha hadi miaka 99 jela kwa kosa la kumchoma Kisu mara mbili baby mama wa NBA Youngboy.
Imeelezwa kuwa tukio hilo lilitokea Jumamosi wiki iliyopita baada ya Iyanna kuwasili nyumbani kwa mpenzi wake Young Boy ambapo alimkuta baby mama wake huyo aitwaye Lapattra Lashai Jacobs. Iyanna alianza kumwambia Lapattra aondoke nyumbani hapo na Baada ya kuzozana sana walifikishana hadi jikoni ambapo binti huyo wa Floyd alichukua visu viwili, pale Lapattra alipozidisha hatua tu, Iyanna alimchoma kisu kimoja.
Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast, Iyanna alishtakiwa kwa kosa la kushambulia mtu na silaha ya hatari, kosa la jinai ambalo linabeba faini ya ($10K) TSH. Milioni 22 au Kifungo cha miaka 99 Jela. Kwa sasa yuko nje kwa dhamana ya TSH. Milioni 68.
ULIIKOSA HII YA UJUMBE WA KIMAPENZI WA NANDY KWA BILLNAS BAADA YA KUVISHWA PETE YA UCHUMBA BASI BONYEZA PLAY HAPA