Leo May 08 2020 Kundi maarufu la muziki kutoka bongo la Navy Kenzo wanajiandaa kurudi na ujio wa album yao mpya, ya pili ikiwa ni miaka mitatu baada ya AIM (Above Inna Minute) waliyoitoa mwaka 2017.
Wakali hao wa nyimbo kama KATIKA, KAMATIA, GAME na FELLA wamekuwa kimya kwa muda huku wakiachia kazi moja moja bila mashabiki wao kujua mipango yao kimuziki imekaaje, lakini hivi karibuni watu waliokaribu na wasanii hao wamesema kuna mengi mazuri ya kutegemea kutoka kundi hilo kwani wapo njiani kuachia album yao mpya itakayoonyesha madiliko waliyoyafanya kipindi chote cha ukimya wao.
“Wamekuwa wakishinda studio sana na muda mwingi wamekuwa wakiutumia kurekodi kazi zao mpya. Awali ilitakiwa watoe EP Project lakini kila wakikaa na kupitia stock yao ya nyimbo wakajikuta inawawia vigumu kufanya maamuzi ya kukamilisha EP hiyo na kuwapa mashabiki project yenye nyimbo chache kwani wanahitaji kitu kikubwa sana kutoka kwao kama fidia ya ukimya wao.
Hivyo wazo la kutoa EP kama limewekwa pause kidogo. Sasa hivi nguvu yao kubwa imewekezwa kwenye kuanda a full-project itakayowaridhisha mashabiki kuwa ukimya wao haukuwa wa bure…” Ms Brown ( PR Manager wa Navy Kenzo)
Haijawekwa wazi project hiyo itakuwa na nyimbo ngapi au itaitwaje, ila watu walio karibu na kundi hilo wanasema ni project ambayo itakidhi kiu ya muziki wa Navy Kenzo uliokosekana kwa muda kidogo:
“Unajua Navy Kenzo sio watu wa kelele nyingi, mara nyingi wao huacha muziki wao ufanye hiyo kazi kwa niaba yao. Ila kama ni kurekodi, wanarekodi sana au niseme wamekuwa wakirekodi sana. Ukikaa studio pale kwa Nahreel huwezi kukosa ngoma kali. Wana muziki mwingi sana, kila siku wanajaribu kurekodi vitu vipya na ideas tofauti tofauti mpya ili kupata kitu kilichobora. Hii project mpya ni kazi kubwa sana; kuanzia sound ya muziki, production, vibes, na miondoko yake.
“Ghana ilikuwa experience kubwa sana kwao, connections walizotengeneza kati yao na wasanii wengine walioenda kushiriki kwenye festival hiyo inaonyesha ni jinsi gani walivyo na nafasi ya kufanya vitu vikubwa sana. AFRO NATION GHANA haikuwa tu wao kwenda kuperform bali kutengeneza pia opportunity za kushirikiana katika kazi za muziki na wasanii na maproducer wa kule, na imani wachache wao watakuwepo kwenye album. Wamefanya kitu kikubwa sana kwenye hii project. – Ms Brown ( PR Manager wa Navy Kenzo)
ISIKUPITE HII YA JUX AKIFUNGUKA KUACHANA NA MPENZI WAKE