Club ya Man City itajua hatma ya rufaa yake kati ya June 8-10 2020 kutoka katika Mahakama ya kimichezo ya kimataifa (CAS), Man City wamefungiwa na UEFA miaka miwili kucheza michuano ya Ulaya baada ya kukiuka sheria za matumizi ya fedha (Financial Fair Play.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri February 14 2020 Man City ilitangazwa kufungiwa (2020/21 & 2021/22) kushiriki michuano ya Ulaya ngazi ya club na faini ya pound milioni 24.9 (Tsh bilioni 74.9) kwa kosa la kuvunja sheria za UEFA za leseni ya vilabu na Financial Fair Play.
Hata hivyo kosa jingine lililosababisha adhabu hiyo ni kuwa Man City hawakutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi, Financial Fair Play kwa mujibu wa UEFA ni kuwa sheria inataka vilabu vifanye usajili kulingana na pesa inazozalisha na sio kuliko kiasi inachoingiza.
VIDEO: RAIS TFF ABANWA BILIONI 1 YA RAIS MAGUFULI, AMTAJA MWAKYEMBE