Uwekezaji kwenye fukwe za Ziwa Nyasa Wilayani Kyela unadaiwa kuwa unaweza kuongeza idadi ya Watalii katika Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini na kuinua uchumi wa taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema hayo wakati akikagua miundombinu ya barabara kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa ambapo amewakaribisha watu wenye uwezo kuwekeza kwenye fukwe za ziwa hilo akidai kuwa bado kuna fursa nyingi na adhimu za uwekezaji.