Diwani wa Kata ya Machame Magharibi Wilayani Hai, Mkoani Kilimanjaro, Martin Munisi ameondoa shauri lake katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi la kutaka kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu unaotarakiwa kufanyika mwaka huu kwa sababu ya tishio la ugonjwa wa Corona.
Munisi amesema ameamua kuondoa shauri hilo kutokana na kupungua kwa madhara ya ugonjwa wa Corona tofauti na hali ilivyokua hapo awali alipokusudia kutaka kuahirishwa kwa uchaguzi kutokana na tishio la ugonjwa wa Covid-19.
“Nimeamua kuondoa kusudio hilo kwa sababu madhara ya ugonjwa wa corona yamepungua nchini kutokana na juhudi kubwa ambazo zimefanywa na Serikali kupitia kwa Rais Magufuli ” Munisi