Serikali imeanza mchakato wa kulipa fidia takribani Million 700 kwa wananchi 411 wa Kijiji cha Kidahwe Wilaya ya Kigoma mara baada ya kutoa eneo ambalo linatarajiwa kujengwa kituo cha kupozea mitambo ya umeme wa Gridi ya Taifa kutokea Nyakanazi mkoani Kagera.
Mara baada ya kukamilika kwa mchakato wa ulipaji wa fidia kwa wananchi, mradi huo utaanza ambao utakuwa chachu kubwa ya ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Kigoma katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanda vikubwa kutokana na kuwa na umeme wa uhakika kuliko hivi sasa ambapo umeme unaotumika ni wa mafuta.
Waziri wa Nishati Dkt. Medad Kalemani amezindua zoezi hilo ambalo limesubiriwa kwa takribani miaka 3 tangu eneo hilo kuchukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kinatarijiwa kuanza kujengwa hivi karibuni.