Rais Bolsonaro ambaye mara kwa mara amekuwa akikataa kuvaa barakoa amesema pia amechunguzwa mapafu kwa kutumia kipimo cha picha cha X-ray katika hospitali ya kijeshi kama tahadhari.
”Ninaepuka kuwakaribia watu, kwa sababu nimetoka hospitali kupima COVID-19, lakini najisikia vizuri, Asilimia 90 ya watu watakaoambukizwa hawatokuwa na dalili” Bolsonaro
“Tunachopaswa kufanya ni kutovieneza virusi kwa wengine. Iwapo nitaathirika virusi vya corona, sitokuwa na wasiwasi, itakuwa ni sawa kama kuwa na mafua au homa. Tuheshimu miongozo ya Wizara ya Afya,” Bolsonaro.
Majibu ya vipimo vya Bolsonaro yanatarajiwa kutolewa leo mchana, Rais huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 65, amesema amekuwa akitumia dawa ya hydroxychloroquine, kama hatua za kujikinga.
Vyombo vya habari vya Brazil vimetangaza kuwa Bolsonaro amebadili ratiba yake ya wiki nzima, ingawa wasaidizi wake hawajatoa taarifa yoyote. Brazil ina zaidi ya wagonjwa 1,623,200 wa COVID-19 na zaidi ya watu 65,000 wamekufa kutokana na virusi hivyo.
Via: DW Swahili
UTEUZI MPYA RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA WILAYA NA KUTEUA WENGINE 5