Kampuni ya Marekani ya Oracle imeingia makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara (Business Patner) na kampuni ya China inayomiliki Mtandao wa TikTok ikiwa ni maamuzi ambayo imebidi yafanyike ili kufata agizo la Rais Donald Trump wa Marekani aliyetaka Tiktok iuziwe Wamarekani lasivyo ataifunga isifanye kazi Nchini humo.
Habari hizi za Oracle kuwa business patner na Tiktok zimekuja baada ya Microsoft kutangaza kwamba hawatoinunua tena Tiktok Marekani, vilevile bado mpaka sasa haijawekwa wazi kuna makubaliano gani kati ya Oracle na Tiktok baada ya kuingia ushirika wa kibiashara.
Tiktok umekua Mtandao wa kijamii wa kwanza wa Kichinia kupata umaarufu mkubwa nje ya China ambapo kwenye miezi mitatu tu ya mwanzoni mwa mwaka 2020 app hiyo ilipakuliwa kwenye simu za mkononi (downloaded) mara MILIONI 315 ikiwa ni rekodi ambayo haijawahi kutokea kwa Mtandao wowote wa kijamii kupakuliwa kwa wingi hivyo katika miezi mitatu.
Kampuni ya Oracle ni kampuni ambayo ilianzishwa mwaka 1977 California Marekani na imekua ikijishughulisha na kuuza database software and technology, cloud engineered systems na enterprise software.
KUTANA NA MZEE ERNESTO ANAYEISHI NA WAKE 16, SABA KATI YAO WAMEOLEWA MTU NA MDOGO WAKE
TEKNOLOJIA BALAA… TAZAMA BEGI LINALOTEMBEA LENYEWE