Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amesema chama hicho kimeiandikia barua NEC ili kuweza kuainisha kwa kina, rufaa zilizotolewa na wagombea na zilivyofanyiwa maamuzi pamoja na kuiomba, kuwachukulia hatua wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo kwa kuwaengua wagombea bila kufuata utaratibu.
Mnyika ametoa kauli hiyo Jijini DSM, ambapo amesema Majimbo ya Butiama, Handeni Vijijini, Kavuu, Kwimba, Kondoa Vijijini, Gairo, Morogoro Mjini, Songwe, Ludewa, Msalala, Lupa ni miongoni mwa majimbo ambayo uamuazi wake haujatolewa.
“CHADEMA imekata rufaa zaidi ya 400 za Udiwani lakini mpaka sasa ni rufaa 100 tu ambazo zimetolewa maamuzi suala ambalo linaminya demokrasia, kwa mfano jimbo la Ukerewe msimamizi wa uchaguzi ameanza kuengua wagombea wa udiwani ambao hawakuwekewa pingamizi” Mnyika