Wakati akizingumza na na wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Bashungwa alisema sheria hiyo itakapoanza kutumika changamoto nyingi zitakwisha.
“Niwaambie tu, Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 ambayo imetoa muda mrefu wa media na waandishi kujiandaa ambao unaisha Desemba mwaka huu, tutaanza kuitumia rasmi Januari mwaka 2022, hivyo kama kuna ambao hawajakidhi matakwa ya sheria hiyo wahakikishe kabla ya Januari hiyo wanakuwa na vigezo, tukianza kuitumia itaondoa changamoto nyingi zinazowakabili,’’ Bashungwa.
Amesema kwa upande wa waandishi wa habari sheria hiyo inawataka ili kufanya kazi ya uandishi wa habari, lazima mhusika awe na sifa ya elimu angalau kuanzia ngazi ya stashahada kutoka vyuo vinavyotambulika na katika kuhakikisha kigezo hicho kinafikiwa, serikali ilitoa miaka zaidi ya minne kwa wasio na sifa kujiendeleza.
“Sheria inamtambua mwandishi wa habari kuwa ni yule mwenye sifa kuanzia ngazi ya Diploma, na kwa kutambua baadhi hawana, wana sifa za cheti tu ulitolewa muda wa mpito kujiandaa pamoja na wamiliki wa vyombo hivyo ili na yale wanayowahusu wahakikishe wanatimiza vigezo, tukianza hatuna mchezo,’’ Bashungwa.