Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumfikisha Mahakama SHADRACK KAPANGA (34), Msaidizi wa kazi za ndani (House boy) kwa kosa la kuwauwa wanafamilia.
‘Jeshi la Polisi kanda maalum ya DSM tarehe 11 June lilimkamata mtuhumiwa SHADRACK KAPANGA (34) akituhumiwa kufanya makosa makubwa ya mauaji eneo la Masaki DSM lililopo wilaya ya Kinondoni, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na baadhi ya vitu alivyoiba akiwemo, TV, Simu, king’amuzi na baadhi ya vitu ambavyo alikuwa tayari kuondoka katika jiji la DSM’- Jeshi la Polisi
‘Baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo alihojiwa na timu yetu na kukiri kufanya kosa hilo kisha kuelekea katika eneo husika kisha kukuta mauaji hayo yamefanyika ya wanafamilia watatu waliofariki akiwemo EMILLY MUTABOYERWA (Mama) na wanae DANIELA MUTABOYERWA (15) na DAMITA MUTABOYERWA (13)’- Jeshi la Polisi
‘Uchunguzi wa awali walikutwa wamepigwa na vitu vizito kichwani, upelelezi wa shauri hili limebaini kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kufanya tukio hilo aliwafungia ndani kisha kuondoka, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani ili kujua sababu ama chanzo cha vifo hivi vya ukatili’– Jeshi la Polisi
SAKATA LA HOUSE BOY ANAYEDAIWA KUUA MAMA NA WATOTO WAKE, WENZAKE WAFUNGUKA “ANAINGIA USIKU”